Mikwara ya Nyota mpya wa Klabu ya Azam FC, Samuel Afful kutoka Ghana.Nyota mpya wa Klabu ya Azam FC, Samuel Afful, ameweka wazi kuwa kikosi hicho kitakuwa moto kuelekea michuano mbalimbali itakayoshiriki kuanzia mwezi ujao kutokana na ujio wake na aina ya wachezaji aliowaona ndani ya timu hiyo.

Mshambuliaji huyo kutoka Ghana amesaini mkataba wa miaka mitatu juzi akitokea timu ya Sekondi Hasaacas ya huko, anaungana na nyota wengine Waghana waliosajiliwa na Azam FC msimu huu, beki wa kati Daniel Amoah, winga Daniel Atta Agyei na mshambuliaji Yahaya Mohammed.

Afful, 20, alifunga bao kwa shuti kali kwenye mechi yake ya mwisho ya majaribio dhidi ya Ruvu Shooting Jumatatu iliyopita katika ushindi wa 3-1 wa Azam FC.

Afful amesema kwa aina ya wachezaji ambao Azam FC imewasajili kutoka Ghana akiwemo yeye basi itarajia kuwa na safu tishio ya ushambuliaji kwenye mechi zinazokuja.

“Nimefurahi sana kujiunga na Azam FC kama mchezaji mwingine anavyofurahia kusaini mkataba na timu mpya, namshukuru Mungu kwani yeye ndiye amefanikisha hili, nimejiandaa vilivyo kuisaidia timu hii na naamini kwa namna nilivyowaona wachezaji kwenye mechi mbili nilizocheza na usajili uliofanywa Azam FCitakuwa moto sana kwa mechi zinazokuja na eneo la ushambuliaji litakuwa tishio,” alisema Afful kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwa vyombo vya habari.
Post a Comment
Powered by Blogger.