Mchezaji wa Uingereza amevuja mkataba na klabu yake ya Rangers.Mchezaji wa Uingereza Joey Barton ambaye haishiwi visa amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba na klabu yake ya Rangers, inayoshiriki ligi kuu ya nchini Scotland.
Barton mwenye miaka 34, mkataba wake ulikua unamalizika mwaka 2018, na ameichezea Rangers michezo nane toka ajiunge na timu hiyo akitokea klabu ya Burnley, mwezi Mei mwaka huu.

Huu ni ujumbe wa Joey Barton katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter


Mchezaji huyu alifungiwa muda wa wiki sita na timu yake baada kutokea mabishano katika mazoezi mwezi Septemba, pia amekua matatani kufuatia tuhuma za kukiuka sheria na uchezaji Kamari, na anachunguzwa na chama cha soka cha Scotland.

Zamani alisha wahi kuvichezea vilabu vya Manchester City, Newcastle, Marseille na QPR, amewashukuru mashabiki wa Ranger, na kuitakia timu hiyo mafanikio.

Post a Comment
Powered by Blogger.