Mcheza tenisi mahiri Maria Sharapova aula UN.Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP, limempa ulaji mcheza tenisi mahiri, Maria Sharapova baada ya kumtangaza kuwa balozi wake wa matumaini pindi adhabu yake ya kufungiwa kwa matumizi ya dawa za kuongeza nguvu itakapomalizika Aprili mwakani.
Sharapova alipewa adhabu ya miaka miwili mapema mwaka huu kwa matumizi ya dawa hizo aina ya meldonium, lakini mwanzoni mwa  Oktoba mwaka huu ikapunguzwa na kubaki miezi 15.
Bingwa huyo mara tano wa michuano ya Grand Slam, aliporwa ubalozi huo wa  UN baada ya kufungiwa lakini sasa ataendelea na kibarua hicho baada ya kurejea uwanjani.
Post a Comment
Powered by Blogger.