Maneno ya Sergio Aguero kuhusu yeye kuwa na ugomvi na Kocha Pep Guardiola..Sergio Aguero amesema hajawahi kuwa na tatizo na kocha wake Pep Guardiola na anaelewa uamuzi wake kumweka benchi.
Mshambuliaji huyo wa Manchester City alianzia benchi kwenye mechi yao dhidi ya Everton na Barcelona, jambo lililosababisha tetesi kwamba huenda akawa na ugomvi na Guardiola.
Ingawa Aguero amesema sababu ya kuwekwa benchi ni kutokana na kichwa chake kutokuwa vizuri baada ya kukosa penalti katika mchezo wa kufuzu fainali za Kombe la Dunia kati ya timu yake ya Taifa ya Argentina dhidi ya Paraguay.
“Sijawahi kuwa na tatizo na Guardiola na hana tatizo na mimi. Siku zote ananisaidia na kunishauri,” alisema Aguero akizungumza na redio ESPN ya Amerika Kusini.
“Baada ya mechi dhidi ya Paraguay, sikuwa vizuri kiakili. Guardiola amenisaidia sana, aliniambia nisifikirie sana tukio hilo na kuijenga akili yangu kwenye kuwazia ushindi.
“Kwa sasa niko vizuri Manchester City, wakati nitakapoondoka kwenye klabu hiyo nitarejea kwenye klabu yangu ya zamani ya Independiente. Kwa muda gani kumekuwa na tetesi za kwenda Real Madrid? Nina furaha kuwepo Man City na zaidi sana kuwa na Pep.”
Post a Comment
Powered by Blogger.