Kocha Jose Morinho ashitakiwa na FA kwa utovu wa nidhamu..


Chama cha mpira wa miguu cha England FA kimemshtaki kocha Jose Mourinho kwa utovu wa nidhamu alioonesha katika mechi ya Man United dhidi ya Burnley jumamosi ya, Oktoba 29,2016.

Imeripotiwa kuwa kipindi cha mapumziko Kocha huyo alitumia maneno mabaya kwa mwamuzi Mark Clattenburg,na kipindi cha pili akapelekwa jukwaani kwa mashabiki kutokana na kosa hilo.

Jose alikuwa mkali kwa mwamuzi huyo akidai kwa nini timu yake haikupewa penati pale Matteo Darmian alipochezewa vibaya na Jon Flanagan katika eneo la hatari.

FA imemtaka Jose kujibu shtaka hilo kabla ya siku ya ijumaa ya juma hili.
Post a Comment
Powered by Blogger.