Klinsmann apigwa chini nafasi ya ukocha MarekaniMchezaji wa zamani na meneja wa Ujerumani Jurgen Klinsmann ametimuliwa katika nafasi yake ya ukocha wa timu ya taifa ya Marekani.

Klinsmann, mwenye miaka ya 52 aliyeshinda Kombe la Dunia akiwa mchezaji mwaka 1990 alianza kukinoa kikosi cha Marekani mwaka 2011, na mafanikio makubwa ambayo ameleta kwa timu hiyo ni kuifikisha hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia, mwaka 2014, nchini Brazil.

''Tunaendelea kuwa imara, tuna wachezaji wa kiwango cha juu wa kutusaidia kufuzu Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi,'' amesema Rais wa Shirikisho la Soka nchini Marekani Sunil Gulati.
Post a Comment
Powered by Blogger.