Klabu ya Yanga kuchuana vikali na Ruvu Shooting katika Dimba la uhuru

img_0035-1

Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea leo kwa mchezo mmoja kupigwa katika uwanja wa uhuru jijini Dar es Salaam.
Mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya Yanga watakua wenyeji wa Ruvu Shooting.Vinara wa ligi hiyo Simba walipoteza mchezo jana huko mkoani Mbeya dhidi ya Tanzania Prison kwa mabao 2-1 na kuwa mchezo wao wa pili kupoteza.

Msimamo wa ligi ulivyo sasa Simba wanaongoza ligi wakiwa na alama 35, huku wakiwa wamecheza michezo 15, Yanga wako nafasi ya pili kwa alama 30 wakiwa wamecheza michezo 14.

Azam ana alama 25 nafasi ya tatu huku wakiwa wamecheza michezo 15. Kagera Sugar wana alama 24 kwa michezoi 15 wako nafasi ya nne.
Post a Comment
Powered by Blogger.