Jeraha la Goti kumweka nje ya soka kwa jumla ya Mwaka mzima.Mchezaji wa klabu ya Hull City, Will Keane hatocheza soka kwa miezi 12 baada ya kupata jeraha la goti.
Keane ambaye anamiaka 23, alipata jeraha hilo katika mechi dhidi ya Southampton ambayo iliisha kwa kupata ushindi wa mabao 2-1 na atafanyiwa upasuaji siku ya Jumanne.

Mshambuliaji huyo aliejiunga na Hull City kutoka Manchester United mwezi Agosti amecheza mechi 6 kwa upande wa kocha Mike Phelan.

”Kumpoteza mchezaji wenye kiwango kama cha Will kwa muda mrefu ni pigo kubwa ”, Phelan ameiambia tovuti ya klabu hiyo.

Hull ambayo ipo katika nafasi ya 18 katika ligi ya premia , pointi moja nyuma ya WestHam.
Post a Comment
Powered by Blogger.