IHF yawanoa nyota wa mpira wa mikono nchini Uganda.Rais wa Shirikisho la Mchezo wa Mpira wa Mikono nchini Uganda, UHF, Shirah Agonzibwe Richardson, ameililia Serikali kupitia Baraza la Michezo la NCS, kuboresha miundombinu ya mchezo huo, nchini humo.
Richardson, amesema hayo baada ya kumalizika mafunzo ya wachezaji 28 ya mchezo wa mpira wa mikono, kambi iliyokuwa ikifanyika kwa wiki moja kwenye fukwe za Entebbe.

Mafunzo hayo yalisimamiwa na mkufunzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Mikono Duniani, IHF, Francisco Aguilera, kutoka Hispania, na kuridhishwa na vipaji vya Uganda, lakini akitaka viendelezwe, ili kufikia lengo la kukuza mchezo wa mpira wa mikono nchini Uganda.
Post a Comment
Powered by Blogger.