Golikipa wa zamani wa Arsenal atinga mahakamani kukata rufaa
Golikipa  wa zamani wa Arsenal na timu ya taifa ya Ujerumani, Jens Lehmann, amekata rufaa kupinga faini ya euro 214,000 baada ya kukutwa na hatia ya kujeruhi.
Lehmann alipinga kutozwa faini hiyo mahakamani jana, baada ya kukutwa na hatia ya kumjeruhi dereva mmoja katika tukio lililotokea maili 18 kusini mwa mji wa Munich, Novemba mwaka 2014.
“Sikumtishia wala kumkaba yeyote,” alisema Lehmann, ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa soka katika kituo cha television cha RTL.
Lehman, aliyeichezea Arsenal mechi 148 na timu yake ya taifa mechi  61 kati ya mwaka 1998 hadi 2008, ametozwa faini hiyo kutokana na makadirio ya mshahara wake wa siku 60 .
Mlinda mlango huyo aliyemrithi David Seaman ndani ya klabu hiyo, atakumbukwa kwa kuiongoza Arsenal kunyakua taji la Ligi Kuu ya England msimu wa 2003-04 bila kufungwa mchezo wowote (Invincibles).
Post a Comment
Powered by Blogger.