Chama cha Kuogelea Tanzania TSA chaomba msaada.
Chama Cha Kuogelea nchini TSA kimeomba wadau wa mchezo huo kujitokeza kusaidia miundombinu ya mchezo huo ili makocha wa mchezo huo waweze kufaidika pindi wanapomaliza kozi mbalimbali za mchezo huo.Katibu Mkuu wa TSA Ramadhani Namkomveka amesema, kwa sasa wanaendelea na kozi ya kitaifa ya mchezo wa kuogelea inayohusisha makocha kutoka mikoa ya Tanzania bara na visiwani lakini mwisho wa kozi hiyo makocha hao wanakuwa hawana sehemu ya kuendeleza elimu waliyoipata kutokana na uhaba wa miundombinu hivyo iwapo wadhamini watajitokeza wanaamini mchezo huo utakuwa zaidi hapa nchini.

Namkomveka amesema, kozi hiyo iliyoanza Novemba saba mwaka inatarajiwa kumalizika Novemba 17 huku ikishirikisha washiriki kutoka mikoa ya Tanzania Bara ambayo ni Mwanza, Singida, Arusha, Kilimanjaro na wenyeji Dar es Salaam huku kutoka Zanzibar ikishirikisha Pemba na Unguja.
Post a Comment
Powered by Blogger.