#BreakingNews: Rais Magufuli avunja bodi ya wakurugenzi TRARais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Mgufuli , leo Tarehe 20 November , 2016 ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Bw.Bernard Mchomvu.

Mbali na kutengua uteuzi huo, Rais Magufuli pia amevunja bodi hiyo kuanzia leo.


Taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imebainisha kuwa uteuzi wa mwenyekiti mwingine pamoja na bodi nzima ya mamlaka hiyo utatangazwa baadaye.
Post a Comment
Powered by Blogger.