Breaking News: Aliyekuwa Spika wa Bunge, Samweli Sitta Afariki Dunia


TANZIA: Aliyekuwa Spika mstaafu wa Bunge na Waziri Mwandamizi Mhe. Samuel Sitta amefariki dunia usiku wa kuamkia leo huko Ujerumani katika hospitali ya Techinical University of Munich, akiwa katika matibabu...


Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, JPM ametuma salam za rambirambi kwa spika wa bunge Job Ndugai kufatiwa kuondokewa na spika mstaafu na mbunge wa  jimbo la urambo mkoa wa Tabora.

Katika salamu hizo Mh. JP Magufuli, amesema ameipokea kwa mshtuuko mkubwa taarifa hiyo ya kifo cha Samweli Sitta, kwa kuwa Taifa limempoteza mtu muhimu aliyetoa toa mchango mkubwa katika uongozi na maendeleo.

"Nitamkumbuka mzee sitta kwa uchapakazi wake, uzalendo wake na tabia yake ya kusimamia ukweli katika kipindi chote alichokuwa kiongozi katika ngazi mbalimbali za siasa na serikali"

"Kupitia kwako mhe. Spika naomba kutoa pole nyingi kwa mke wa marehemu Mhe. Magreth Sitta Ambaye ni mbunge wa jimbo la urambo na familia nzima ya marehemu, Wabunge wa bunge laa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Wananchi wa Urambo mkoani Tabora na watu wote walioguswa na msiba huu." Amesema Rais Magufuli katika salamu hizo.

 Poleni ndugu , jamaa na marafiki wote na Mungu ailaze Roho ya Marehemu mahala pema peponi Amina.
Post a Comment
Powered by Blogger.