Beki wa Manchester united Matteo Darmian njiani kutimkia Italy.Mchezaji wa klabu ya Man Utd na timu ya taifa ya Italia, Matteo Darmian ambaye hucheza nafasi ya beki wa pembeni Darmian huenda akarejea nyumbani wakati wa dirisha dogo la usajili, kufuatia meneja mpya wa Inter Milan Stefano Pioli kuonyesha dhamira ya kutaka kumsajili.

Darmian mwenye umri wa miaka 26, amekuwa hapati nafasi ya kuanza katika kikosi cha Man Utd chini ya utawala wa kocha Jose Mourinho,hivyo inaaminiwa huenda ikawa njia rahisi kwa Inter Milan kumsajili kwa mkopo itakapofika mwezi januari.

Kama Inter Milan watafanikiwa kumsajili Darmian kwa mkopo, huenda wakapendekeza kumchukua jumla itakapofika mwishoni mwa msimu huu.

Man Utd walimsajili Darmian mwaka 2015 kutoka klabu ya Torino, hadi sasa ameshafanikiwa kucheza michezo 30 ya michuano yote.
Post a Comment
Powered by Blogger.