Azam FC kukosa huduma ya beki wake Shomari Kapombe michezo yake yote mitatu ya Kanda ya Ziwa,..AZAM FC imethibitisha kuwa itakosa huduma ya beki wake wa kulia, Shomari  Kapombe, katika michezo yake yote mitatu ya Kanda ya Ziwa.
Tayari Kapombe aliukosa mchezo wa mwishoni mwa wiki iliyopita wakati Azam ilipoibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba.
Daktari wa Azam FC, Mwanandi Mwakemwa, alilithibishia Gazeti la Bingwa jana kuwa beki huyo anayeuguza nyama za paja ataukosa mchezo wa kesho dhidi ya Toto Africans.
“Kapombe bado anauguza majeraha yake ya nyama za paja ambayo yatamfanya kuwa nje ya uwanja katika kipindi cha wiki mbili, muda wote huo atakuwa chini ya uangalizi wa jopo la madaktari,” alisema.
Kuelekea mchezo dhidi ya Toto, Meneja wa Azam, Philipo Alando, amesema wachezaji wao wapo katika hali nzuri kimwili na kiakili kuelekea mchezo huo.
“Kama tulivyowaahidi mashabiki wetu kuondoka na pointi 12 Kanda ya Ziwa, wembe tuliotumia kumnyoa Kagera ndio utakaotumika kumnyoa Toto Africans,” alisema.
Post a Comment
Powered by Blogger.