Upotevu wa milioni 114 wawaweka ndani viongozi wa SACCOS Ludewa


Mkuu wa wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Andrea Tsere, amewaweka ndani Meneja na Mwenyekiti wa bodi ya Saccos ya Mlangali na kuivunja Bodi yake na kutoa siku 30 kwa Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa Upotevu wa milioni 114
Mkuu huyo wa Wilaya pia ameagiza wanachama wa Saccos hiyo kulipa deni la marehemu ambaye alikuwa meneja wa awali aliyefariki kwa kujinyonga mwaka 2012.

Maamuzi hayo yanakuja baada ya kuwepo kwa sintofahamu ya matumizi ya fedha za wanachama na fedha nyingine kulipa hasara iliyosababishwa na marehemu.

Mwenyekiti wa muda wa Saccos hiyo Nasanael Mgani anasema kuwa katiba ya Saccos hiyo ilikiukwa na uongozi wa marehemu na wa sasa kwa kuwa katiba ya chama hicho haikutumika.

Wanachama wa chama hicho wanasema kuwa uamuzi ulio chukuliwa utasaidia kurejeshwa kwa fedha zao.
Post a Comment
Powered by Blogger.