Timu ya soka ya Arsenal imevipita vilabu hivi vikubwa kipesa ..


Licha ya kutochukua ubingwa wa Ligi Kuu England kwa zaidi ya miaka 10, usidhani klabu ya Arsenal iko vibaya katika masuala ya kiuchumi.
Kwa mujibu wa taarifa za kifedha zilizotolewa na Arsenal, klabu hiyo ina pauni milioni 226.5 kwenye akaunti yake ya benki.
Kwa kiasi hicho kwenye akaunti, klabu hiyo ya jijini London imezipiku Real Madrid, Barcelona na Bayern Munich.
Hata hivyo, Arsenal iko nyuma ya wapinzani wao, Manchester United, ambao hivi karibuni walidai kuwa akaunti yao ya benki ina pauni milioni 229.
Hata hivyo, wakati Man United ikitangaza kuwa na kitita hicho benki, ilikuwa ikikabiliwa na madeni.
Akizungumzia mafanikio hayo ya kiuchumi, Mkurugenzi wa Arsenal, Sir Chips Keswick, alisema: “Akiba yetu ya kifedha mwishoni mwa mwaka jana ilikuwa pauni milioni 226.5 na huenda mapato haya yakawavutia mashabiki.”
Wachambuzi wa masula ya kiuchumi wameelezea kuongezeka kwa kipato cha Arsenal, wakidai kuwa hilo limetokana na mkataba mnono wa haki ya matangazo ya televisheni.
Kwa upande wake, Mtendaji Mkuu wa Gunners, Ivan Gazidis, amedai kuwa wataendelea kujipanga na kuhakikisha wanapiga hatua zaidi.
“Uwanjani tuna kikosi imara. Nje ya uwanja tumeboresha miundombinu yetu kuhakikisha tunasonga mbele kutoka hapa tulipo.
“Lengo letu ni moja na liko wazi: Ni kushinda mataji makubwa na kuifanya Arsenal kuwa timu kubwa,” alisema bosi huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.