Tetesi za kutimuliwa kwa Kocha wa Inter Milan, Frank de Boer amezizungumzia..
Kocha wa Inter Milan, Frank de Boer, amesema amechoshwa na taarifa za mara kwa mara kuwa atatimuliwa klabuni hapo.

Kumekuwa na taarifa kuwa Mholanzi huyo atapokonywa kibarua cha kuliongoza benchi la ufundi kutokana na mwenendo wa kusuasua wa kikosi hicho.

“Nimechoka kuzungumzia suala hili. Jambo pekee linalonihusu kwa sasa ni timu. Ni wakati mgumu kwangu, kwa timu, na kwa kila mmoja, lakini tunatakiwa kuungana kurekebisha hali ya mambo,” alisema De Boer.
Post a Comment
Powered by Blogger.