Tambo za kocha Jose Morinho kuelekea mechi na Liverpool..


Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema mchezo wao dhidi ya Liverpool ni wa kawaida kama ilivyo mechi nyingine zinazokutanisha timu mahasimu.

Mourinho atakuwa na vijana wake Jumatatu kwenye Uwanja wa Anfield kucheza na Liverpool katika kinyang’anyiro cha EPL.

Bosi wa Liverpool Jurgen Klopp amesema pambano hilo lisikuzwe sana, lakini Mourinho kwa upande wake amesema kwamba, uhasama wa timu hizo sio mkubwa kama ule ambao amewahi kukutana nao katika sehemu tofauti za maisha yake ya ukocha.

Amesema; “Mara nyingi nimekuwa nikipenda kucheza Anfield. Nimeshinda mechi kubwa na kupoteza mechi kubwa pia. Si kweli kwamba mara zote nimekuwa nikipata mafanikio lakini napenda sana kwenda pale, naipenda sana hali iliyopo pale na kingine ni tabia za mchezo huo.”

“Kuwa meneja wa Manchester United ni dhahiri kuna maana kubwa sana, lakini kwangu mimi huo ni mchezo mkubwa tu. Unaweza kuwa sawa na ule wa AC Milan na Inter Milan, Real Madrid-Barcelona, na pengine Porto-Benfica.”

Mourinho amemfunga Klopp kwenye mchezo mmoja tu kati ya mitano waliyokutana ambao ulikuwa wakati yupo Real Madrid aliposhinda mabao 2-0 dhidi ya Borussia Dortmund kwenye mchezo wa Champions League

“Sina la kuongea zaidi,” hilo ni jibu alilotoa baada ya kuulizwa juu ya kazi ya Klopp anayoifanya Liverpool.

Alipoulizwa kama Liverpool ni moja ya timu zinazopigania ubingwa, aliongeza: “Hilo swali waulizeni wenyewe. Ni timu nzuri.”
Post a Comment
Powered by Blogger.