Siri ya Stand United kuzichapa Yanga na Azam Kambarage Shinyanga...

Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bilal ametaja siri ya timu yake kuibuka na ushindi dhidi ya timu za Yanga na Azam FC kuwa ni kutokana na kuwajenga kisaikolojia wachezaji wake.

Akizungumza na Gazeti la Michezo kubwa hapa Tanzania Bilal alisema kabla ya mchezo huo aliwapa somo wachezaji wake kwa kuwataka wasibabaishwe na majina ya wapinzani wao.

Alisema dhamira yao ni kuhakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu msimu huu na uwezo wa kufanya hivyo wanao kwakua kikosi chao kina wachezaji wanaocheza kwa uelewano mkubwa.

“Mbali na kuwafundisha mbinu za ushindi na namna ya kulinda bao endapo wakifanikiwa kutangulia kufunga huwa naawambia wasiangalie ukubwa wa majina ya timu wanazokutana nazo kwani nao ni wachezaji kawa wao, hivyo hakuna haja ya kuwaogopa.

Hakika hii imekuwa silaha kubwa na ndio maana Azam na Yanga tumewafunga katika uwanja wetu wa nyumbani,” alisema Bilal.

Kocha huyo alisema,wanaupa umuhimu mkubwa kila mchezo ulioko mbele yao na ndio maana wamefanikiwa kushinda michezo mitano na kutoka sare nne
Post a Comment
Powered by Blogger.