Simba na Yanga Wazuiwa Kutumia Uwanja Wa Taifa


Timu za soka za Simba na Yanga za Jijini Dar es Salaam zimezuiwa kutumia Uwanja wa Taifa kwa muda usiojulikana kutoka na mashabiki wao kusababisha uharibifu wa miumbombimu ya Uwanja  wa Taifa yakiwemo mageti ya kuingilia Uwanjani na kung’oa viti kwa upande wa mashabiki wa Simba.

Tamko hilo limetolewa na Serikali hivi punde baada ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kulieleza hilo wakati akizungumza na waandishi wa habari.

“Uwanja huu sasa hautatumika na Yanga na Simba, hawawezi kufanya uharibifu huu wa makusudi huku wakijua kwamba uwanja huu ndani yake kuna kodi za walipa kodi.

“Mmeona walichofanya na sasa wanaweza kutafuta sehemu ya kwenda kucheza, watafute uwanja wa kutumia, hadi hapo tutakapoamua vinginevyo,” alisema Nape.

“Wanaotakiwa kuutumia ni ukiwa mzuri na si kama ulivyo sasa, wako wengine wastaarabu wanaweza kuutumia.”

Mashabiki wa Simba waling’oa viti na kuvirusha uwanjani baada ya Amissi Tambwe wa Yanga kufunga bao na kabla ya kufunga alikuwa ameshika lakini mwamuzi hakuchukua uamuzi wowote. Lakini mashabiki wa Yanga nao wakajibu mapigo ya kurusha viti baada ya Simba kusawazisha bao katika dakika ya 87 kupitia Shiza Kichuya.

Kwa hatua hiyo ya Serikali kuzuia kutumiwa uwanja huo timu za Dar es salaam zinatakiwa kutafuta viwanja vya kutumia kwa mujibu wa kanuni ya sita ya Ligi Kuu kuanzia vipengele vya 1-6.

Post a Comment
Powered by Blogger.