Shiza Kichuya aibuka mchezaji bora wa mwezi Septemba ligi kuu bara..Jumapili ya October 13 2016, Makamu wa Rais wa Simba Kaburu alimkabidhi tuzo ya mchezaji bora wa klabu wa mwezi September mchezaji Shiza Kichuya kabla ya mechi dhidi ya Toto Africans.

Kichuya alisaidia mechi zilizo pita Simba kupata ushindi na kufunga magoli na kusaidia magoli mengine kufungwa alifunga mabao matatu katika mechi mbili kati ya nne ambazo alicheza.

Simba SC iliibuka na ushindi wa 3-0 Toto Africans hivyo kufikisha pointi 29 baada ya kucheza mechi 11 na sasa wanawazidi mabingwa watetezi, Yanga walioa nafasi ya pili kwa pointi nane.

Post a Comment
Powered by Blogger.