Sababu za Joseph Owino kuipa nafasi ya Simba timu ya Stand United msimu huu..Beki wa zamani wa Simba na Timu ya Taifa ya Uganda, Joseph Owino, ameitabiria makubwa Stand United, baada ya kusema timu hiyo ina nafasi ya kumaliza msimu ikiwa kwenye nafasi ya tatu.

Beki huyo kwa sasa anaichezea timu ya Fanja FC, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Oman.

Kabla ya kusaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea Fanja FC, Owino aliitumikia Stand United kwa kipindi kifupi katika Ligi Kuu inayoendelea.

Akizungumza na Gazeti marufu la kimichezo hapa Tanzania, Owino amesema licha ya mgogoro uliopo katika klabu hiyo ukihusisha pande mbili zinazopingana, bado timu hiyo inaweza kufanya makubwa msimu huu kutokana na ubora ilionao.

“Ukiondoa mgogoro uliopo ndani ya timu, Stand wana kikosi bora ambacho kina uwezo wa kumaliza ligi kikiwa katika nafasi za juu kama nafasi ya tatu.

“Kikubwa ni wachezaji kujua majukumu yao na kuacha kusikiliza migogoro ya kiuongozi ambayo haina faida kwao, wao wanatakiwa kufanya kazi yao ambayo ni kucheza mpira na kuipa matokeo,” alisema Owino.

“Naamini hilo likifanyika timu ina nafasi ya kumaliza katika nafasi ya tatu.”

Katika msimamo wa Ligi Kuu Bara, Stand United ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 15, nyuma ya Simba inayoongoza ikiwa na pointi 17.
Post a Comment
Powered by Blogger.