Angalia Ndege Nyingine Mbili Ambazo Serikali itazinunua Mwakani - JPMBaada ya serikali kupitia juhudi za rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania mh. Dk. Magufuli, kununua ndege mbili mpya bombardier Q400,hatimaye JPM hajakata tama na kuahidi kuendelea kuleta ndenge nyingine.Juzi katika hotuba ya uzinduzi wa ndege mpya aina ya Bombardier Q400; Rais Magufuli ametamka kuwa Serikali yake ina mpango wa kununua ndege nyingine mbili mpya za injini ya Jet.


Ndege hizo moja itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 160 na nyingine itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 240. Ndege hizo si nyingine bali ni Airbus A320 na Airbus A330-200. Embu tuzitazame hizo ndege kiundani zaidi:
         
                                                   Airbus A320

Ndege hii ina uwezo wa kubeba kati ya abiria 150 hadi 180 katika mpangilio wa madaraja matatu. Ina uwezo wa kwenda hadi umbali wa 6,500 km kwa kasi ya 871 km/h bila kutua na inatumia injini aina ya CFM56-5 au IAE V2500-A5
 Bei ya hii ndege ni US $98.0 milioni 


                                                       Airbus A330-200
 
Ndege hii ina uwezo wa kubeba abiria 247 katika mpangilio wa madaraja matatu. Ina uwezo wa kwenda hadi umbali wa 13,450 km kwa kasi ya 913 km/h bila kutua na inatumia injini aina ya PW4000, Rolls-Royce Trent 700 au GE CF6-80E1.
Bei ya hii ndege ni US$231.5 milion
Post a Comment
Powered by Blogger.