Navy Kenzo Waipeperusha Tena Bendera Ya Tanzania

KUNDI la Muziki wa Bongo Fleva, linaloundwa na wapendanao, Aika Mareale ‘Aika’ na Emmanuel Mkono ‘Nahreel’ limeitoa kimasomaso Bongo baada ya kutangazwa kama kundi pekee kutoka Bongo kushiriki kwenye Msimu wa Nne wa Coke Studio Afrika utakaoanza hivi karibuni kuruka kupitia vituo mbalimbali vya televisheni
 
Katika msimu huu nchi sita zimeongezwa ambazo ni Ivory Coast, Cameroon, DRC Kongo, Ghana, Senegal na Ethiopia ambapo wasanii wapya walioingia kushirikiana kwenye kolabo ni pamoja na Kiss Daniel na Patoranking (Nigeria), Bahati (Kenya), Eddy Kenzo pamoja na Redio na Weasel kutoka Uganda. Wasanii wengine ni Kundi la Navy Kenzo (Bongo), Toofan (Togo) na Haile Roots kutoka Ethiopia.

 

Vile vile First lady wa kundi hilo AIKA  amezidi kuwakumbusha wadau wamuziki Tanzania pamoja na Afrika kwa ujumla kuwapigia kura ktk tuzo za MTV MAMA kama Best group kutoka Afrika  

Post a Comment
Powered by Blogger.