Msimamo wa Timu ya soka ya Arsenal kuhusu Mesut Ozil na Alex Sanchez..Timu ya soka ya  Arsenal imesisitiza kuwa wana uwezo wa kuwabakiza kundini nyota wao, Mesut Ozil na Alexis Sanchez.

Wawili hao wanatarajiwa kumaliza mikataba yao mwaka 2018 na wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kuondoka Emirates.

Arsenal walikuwa na utaratibu wa kuwauza wachezaji wao wa kiwango cha juu miaka iliyopita ili kubalasi vitabu vyao vya hesabu.

Lakini Ivan Gazidis anaamini Washika Bunduki hao wanaweza kukabiliana na changamoto kutoka timu nyingine litakapokuja suala la mshahara na watajaribu kwa nguvu zao zote kuwabakiza Ozil na Sanchez kuendelea kuitumikia timu yao.

Kiongozi huyo alisema jana: “Tuna rekodi nzuri katika misimu ya hivi karibuni katika suala zima la kuwauza wachezaji wetu nyota, huku tukiwaendeleza wachanga na kuvutia wengine wapya.

“Kwa sasa tumeanza kupambana katika suala zima la mshahara dhidi ya klabu zinazotuzunguka. Kuna maendeleo makubwa katika uwekezaji hali inayotuwezesha kumudu kukabiliana na ushindani wa mishahara lakini pia dau la uhamisho,” alisema.
Post a Comment
Powered by Blogger.