Miamba hii inamuwania Thiago Silva kumsajili bure mwisho wa msimu...
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Italia, klabu ya Juventus, imeonesha dhamira ya kutaka kumchukua mchezaji mwingine mwenye uwezo wa hali ya juu kwa uhamisho wa bure na beki wa PSG, Thiago Silva, yupo kwenye rada za kibibi kizee hicho cha Turin.

Silva, mwenye umri wa miaka 32, anatarajiwa kumaliza mkataba wake na mabingwa hao watetezi wa Ufaransa mwishoni mwa msimu huu na Mkurugenzi wa Juventus, Giuseppe Marotta, amekuwa wazi juu ya kumsajili beki huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.