Mchezaji wa zamani wa klabu ya West Ham alivyoguswa na Kukaa Bench I kwa Yaya Toure..

Mchezaji wa zamani wa klabu ya West Ham, Dean Ashton, ni kama amekerwa na tabia anayoionesha kiungo wa Manchester City, Yaya Toure tangu msimu huu ulipoanza.

Kiungo huyo wa Ivory Coast aliachwa nje ya kikosi tangu Septemba baada ya wakala wake Dimitri Seluk, kumponda wazi kocha wa City, Pep Guardiola.

Guardiola alisema kwamba, ataanza kumtumia tena Toure mwenye umri wa miaka 33 kama ataomba msamaha kwa niaba ya wakala wake.

Lakini Toure ameonekana kama ni mwenye furaha kukaa benchi akijichotea mshahara wa pauni 220,000 kwa wiki na jambo hilo limemkasirisha mno Ashton.

Ashton alistaafu akiwa na umri wa miaka 26 kutokana na majeraha yaliyomkumba katika wakati mbaya na alisema kama angekuwa yeye ndiye kiungo huyo, angehakikisha anapata nafasi ya kucheza.

“Ni jambo la kushangaza, kichwa changu hakitaki kukubali.

“Ujue, Toure ni kama anasubiri wakati ufike auzwe tu.

“Kama anataka kucheza kweli basi angemwambia wakala wake hivi: ‘Nyamaza, nitaomba msamaha, hata kama sitamaanisha ili tu nipate nafasi ya kucheza.

“Kuna wachezaji wengine ambao hawajisumbui kama alivyo Toure kwa sasa. Lakini kama ana mawazo tofauti basi angeomba msamaha na kucheza.

“Ningekuwa mimi ningefanya lolote nipate angalau mchezo mmoja. Nakereka kuona mambo kama haya ya Toure,” alisema.
Post a Comment
Powered by Blogger.