Mchango wa Diamond Platnumz kwa Said aliesababishiwa matatizo ya macho na Scorpion.Asubuhi ya leo katika kipindi cha Leo Tena chaClouds Fm alikuwepo kijana Said, kijana ambaye tukio alilofanyiwa limewagusa wengi baada ya kutobolewa macho na kijana ajulikanae kama Scorpion.

Ni katika kuendeleza kampeni ya kumuombea mchango kijana huyo kwa yeyote aliyeguswa na tukio hilo ili kuhakikisha kijana Saidanapata matibabu na kurudi katika hali yake ya kawaida kama itawezekana.

Diamond Platnumz ni mmoja kati ya walioguswa vilivyo na tukio hilo, na hakuona vibaya kujisogeza katika ofisi za Clouds Fmasubuhi ya leo ili kukutana na kijana huyo na kuweza kumchangia chochote kidogo alichonacho.

Diamond Platnumz alitoa Tsh. Millioni 2 taslim na kumkabidhi kijana Said kama msaada wake kwa kijana huyo.Diamond Platnumz na ndugu Saidi

Sio Diamond Platnumz pekee ambae alihudhuria studioni hapo, bali pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Muheshimiwa Paul Makonda naye pia alihudhuria na kukabidhi Tsh Million 10 kama kutimiza ahadi yake aliyoahidi kumpa ndugu Said kama mtaji ambao utakuwa kama msingi katika kuendeleza maisha yake baada ya kupatwa na matatizo hayo.

Paul Makonda hakuishia kwenye millioni 10 tu, bali alitaja misaada mingine ambayo imetolewa na makampuni, taasisi pamoja na watu binafsi ambao amewatembelea kumuombea msaada kijana Said. Ambapo alitaja kuwa zimepatikana Pikipiki 5 ambazo zitafanya kazi kama Bodaboda kuhakikisha zinamuingizia kipato cha kila siku ndugu Saidi, Bajaji 2 pamoja na kuahidiwa kujengewa nyumba katika jiji la Dar es Salaam sehemu yoyote ile ambayo ndugu Said atahitaji.

Bado misaada inaendelea kupokelewa kwa yeyote aliyeguswa na hili na hii hapa ni namba ya account ambayo inapokea pesa za misaada ya ndugu Said-:CRDB Bank Account 0152226886400 jina Said Ally
Post a Comment
Powered by Blogger.