Maamuzi Ya Samsung Kuhusu Mauzo Na Madai Ya Kulipuka Kwa Galaxy Note 7

Baada ya kusitisha mauzo yake mwezi mmoja uliopita, kutokana na madai kwamba simu hizo zinalipuka, Samsung imeanza mauzo ya simu yake, Galaxy Note-Seven nchini korea kusini,
Kampuni hiyo inasema hitilafu kwenye betri zake zilisababisha milipuko hiyo.

Takriban simu milioni mbili laki tano zilirejeshwa kutoka maeneo mbalimbali ulimwenguni, ili kupata betri  mpya.
Makampuni ya ndege yamekuwa yakiwaonya abiria wake kutumia simu hiyo ndani ya ndege.
Hata hivyo sio simu zote zilizo na hitilafu kwenye betri zilizorejeshwa,
Samsung inatoa simu za bure kwa wale walioathirika huku wafanyibiashara wa simu hizo wakipata mali mpya huku simu zaidi zikiendelea kufikishwa sokoni.
''Tumetoa wito kwa waathiriwa wa simu hizo kuzibadilisha haraka iwezekanavyo. Simu ya galaxy Note 7 zenye betri ishara ya betri ya kijani zilikuwa salama kutumia'',Imesema Samsung.
Post a Comment
Powered by Blogger.