Kocha wa zamani wa Vital O’ alivyowaonya wanaomponda Mavugo..


Kocha wa zamani wa Vital O’, inayoshiriki Ligi Kuu ya nchini Burundi, Ndayiragije Etienne, amesema mshambuliaji wa Simba, Laudit Mavugo, atafanya mambo makubwa kuliko watu wanavyomtazama kwa sasa.
Kocha huyo, ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Mbao FC cha jijini Mwanza, anaamini Mavugo anaathiriwa na ugeni na kudai kuwa kama atapewa muda zaidi atafanya makubwa na kuwashangaza watu.
Alisema baada ya kumfuatilia mshambuliaji huyo, amebaini kinachomsumbua ni mazingira, hivyo anatakiwa kukomaa ili aweze kuonyesha ubora wake.
“Mwaka jana nilikuwa na Mavugo Vital O, ni mchezaji mwenye kipaji cha hali ya juu na anaweza kufanya mambo makubwa uwanjani kwa muda mfupi, ila kinachompa shida hivi sasa ni uzoefu, mashabiki wampe muda,” alisema.
Alisema Mavugo anaweza kufikia makali ya Tambwe na hata kumpiku kama ataendelea kupewa nafasi ili kuzoea mazingira ya soka la Tanzania.
“Nilimshuhudia Mavugo kwenye mechi kadhaa, ikiwamo ya Mtibwa Sugar, yuko vizuri. Tambwe ameshaizoea ligi hii, tofauti na Mavugo ambaye amekuja msimu huu,” alisema.
Post a Comment
Powered by Blogger.