Kocha wa zamani wa Azam amepata dili nchini Kenya..Kocha wa zamani wa Azam FC, Stewart Hall, amepata ‘shavu’ katika klabu ya AFC Leopard inayoshiriki Ligi Kuu ya Kenya ambayo anachezea straika wa zamani wa Simba, Paul Kiongera.

Hall ambaye alitimuliwa Azam kwa madai ya kushindwa kuendana na kasi ya Wanalambalamba hao, amepewa mkataba wa miaka miwili ambapo atakuwa katika klabu hiyo hadi mwaka 2018.

AFC Leopard inashika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini humo ambapo wenye timu yao wanaona kikosi chao kinaelekea kubaya na kuamua kumpa ulaji kocha huyo ili kuwanusuru na nafasi za chini.

Katika kikosi hicho, Hall anakwenda kukutana na Paul Kiongera ambaye aliachana na Simba baada ya kuona hapati namba na sasa wawili hao watashirikiana ili kukisaidia kikosi chao kupata matokeo mazuri.
Post a Comment
Powered by Blogger.