Kocha Mzambia kuchukua mikoba ya Hans Pluijm.

 
Kocha George Lwandamina kutoka Zambia jana ametua rasmi nchini kwa ajili ya kumalizana na uongozi wa Yanga tayari kuchukua mikoba ya Hans Pluijm anayetajwa kupewa wadhifa wa ukurugenzi wa ufundi.


Licha ya uongozi wa Yanga kuufanya ujio  huo kuwa siri kubwa, uhakika ni kwamba Lwandamina ametua nchini jana mchana na kupelekwa kwenye moja ya hoteli za kifahari jijini Dar es Salaam.

Katika miaka miwili ambayo Lwandamina ameiongoza klabu ya  Zesco United kwenye mashindano ya kimataifa, timu hiyo imecheza  mechi 18 za mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Post a Comment
Powered by Blogger.