Kocha mkuu wa Toto Afrika ya Mwanza abwaga manyanga kwa sababu hii..

unnamed
Kocha mkuu wa timu ya soka ya "Toto African Sports Club" ya Jijini Mwanza, Rogasian Kaijage, amebwaga manyanga kuifundisha timu hiyo kutokana na mwenendo mbovu kwenye ligi kuu ya soka tanzania bara.

Msemaji wa timu hiyo, Cuthbert Japhet, amesema kocha huyo ameachia ngazi baada ya timu ya Toto kuchezea kichapo cha bao 1-0 ikiwa kwenye dimba lake la nyumbani, CCM Kirumba, ilipokuwa ikimenyana na timu ya Ndanda Fc ya mkoani Mtwara.

"Tutawataarifu baadaye hatua tutakazochukua ikiwemo kuwajuza nani atachukua mikoba ya Kaijage, maana ni mapema kuzumzia suala hilo kwani kajiuzulu mwenyewe baada ya mechi ya jana na siyo kwamba tumemfukuza". Japhet.

Kaijage bado hajapatikana kuzungumza anakoelekea baada ya kuachana na Toto, ijapokuwa hali kwake kwani kati ya mechi saba ambazo timu hiyo imecheza kwenye mzunguko wa ligu kuu, imeshinda mechi moja, imetoka sare mechi mbili na kufungwa mechi nne, matokeo ambayo hayakumridhisha kocha huyo na hivyo kuamua kutimka.

Post a Comment
Powered by Blogger.