Klabu ya Soka ya Simba ilivyoendeleza ubabe ligi kuu Tanzania..


Timu ya Simba ya Jijini Dar es salaam imeibuka na alama tatu muhimu katika mpambano wa leo uliofanyika katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es salaam baada ya kuinyuka Kagera Sugar kutoka Kagera kwa magolI mawili kwa bila.

Katika mchezo huo uliokusanya mashabiki wengi kutoka maeneo mbalimbali ulikuwa mgumu kwa pande zote mbili ambapo timu zimeshambuliana kwa zamu ambapo dakika ya 44 ya kipindi cha kwanza mchezaji Muzamil Yassin akaifungia Simba goli zuri kwa shuti kali.

Baada ya mapumziko ya kipindi cha kwanza na kipindi cha pili kurejea kwa timu zote kukamiana Kagera Sugar kitaka kurejesha goli huku Simba nao wakishambulia kwa kasi wakitaka kuongeza goli.

Dakika ya 74 mchezaji Shiza Kichuya akaifungia Simba goli la pili kwa mkwaju mkali wa penati baada ya mchezaji wa Simba Mohamed Ibrahim kudongoshwa eneo la hatari

Mpaka mwisho wa mchezo Simba mbili Kagera Sugar hawajaambulia kitu, ambapo kwa ushindi huo Simba wamezidi kupaa kileleni baada ya kucheza mechi 9 na kushinda mechi 7 na magoli 17 na inaongoza kwa alama 23.

Matokeo mengine ya ligi kuu hii leo ni kama ifuatavyo JKT Ruvu 1-1 Mwadui FC na Stand United 1-1 African Lyon.
Post a Comment
Powered by Blogger.