Kipaji cha Daniel Sturridge kimemgusa kocha wake Jurgen Klopp tizama alichokisema.Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp, amedai kuwa hajawahi kutilia shaka kipaji cha straika wake, Daniel Sturridge, ambaye juzi alipachika mabao mawili katika ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Tottenham.

Mabao ya staa huyo mwenye umri wa miaka 27 ndiyo yaliyoiwezesha Liver kuingia hatua ya robo fainali ya Kombe la Ligi.

Mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Anfield ulikuwa wa kwanza kwa fowadi huyo wa kimataifa wa England tangu alipocheza Agosti.

“Ule ndiyo uwezo wake, ndiyo nguvu yake. Ni mmaliziaji, ni mpachikaji mabao mazuri, hakuna shaka juu ya hilo,” alisema Mjerumani huyo.
Post a Comment
Powered by Blogger.