King kiba Asema Haya Kuhusiana na Mjengo wake


Msanii kutoka Lebo ya Rockstar 4000, Alikiba  Amegoma kumiliki mjengo mkali uliopo maeneo ya Tabata ambao baadhi ya wadau  kuufananisha mjengo huo na Ikulu ya Morocco, licha ya yeye mwenye ku post picha za mjengo huo jana usiku kwenye mitandao ya kijamii ukiwemo instagram.

King kiba amezitolea nje stori hizo za kumiliki mjengo huo wa kifahari wakati akihojiwa na mmbea wa kimataifa Soudy brown katika kipindi cha U-Heard cha Clouds fm, na kugoma kabisa kuongelea kuhusiana na hilo.

Licha ya hilo Msanii mkongwe kwajina la H-Baba alitokwa na povu zito baada ya majibishano ya mijengo katika ya Diamond na Alikiba. Ambapo baada ya King kiba ku post mjengo huo nae Diamond alipost mjengo wake na majungu ya kutosha kurushwa kwenye mitandao ya kijamii.

Ambapo msanii H-Baba aliwataka kupongezana na sio kurushiana vichupa vya majungu, na vile vile kusema eti kama kweli unamuliki nyumba atume pesa akiwa anasaidi kununua nyumba au Kupost hati ya nyumba hiyo.....MI sipo ni Umbea kutoka hukooo kwenye mitandao ya kijamii na kwa Gossip Cop


Post a Comment
Powered by Blogger.