Isha Mashauzi na Leyla Rashidi kuchuana vikali ndani ya Dar live.


Jahazi na Mashauzi Classic kusindikiza WAIMBAJI wawili wanaokimbiza kwenye soko la taarab kwa hivi sasa Isha Mashauzi na Leyla Rashid watapambana vikali Oktoba 22 ndani ya ukumbi Dar Live Mbagala.
Unaambiwa ni malkia wawili ndani ya jukwaa moja, ambapo Isha Mashauzi atathibitsha kuwa nyeye ni malkia wa masauti matamu huku Leyla akitaka kudhihirisha kwamba yeye ndiye malkia wataarab.
Mratibu wa onyesho hilo Hajji Mabovu amesema bendi mbili kubwa za taarab Jahazi Modern Taarab na Mashauzi Classic zitasindikiza mpambano huo wa Isha na Leyla.
Waimbaji hao wawili kwa pamoja wameuthibitisha kuwa wamefikia makubaliano ya kuonyeshana ubabe Jumamosi yatarehe 22 mwezi huu.
Leyla Rashid amesema anamsikitikia sana Isha Mashauzi kwakukubali kushiriki mpambano huo kwa vile kwasasa yeye (Leyla) nimaji marefu ambayo kamwe Isha hawezi kuyagoka.
Naye Isha Mashauzi ametamba kuvuna ushindi mkubwa na kuongezakuwa Leyla ameingia choo cha kiume kwa kukubali mtanange huo.
Post a Comment
Powered by Blogger.