Golikipa Joe Hart kwenye harakati za kurejea Ligi kuu Uingereza..


Timu ya Chelsea inasemekana kumfukuzia mlinda mlango wa Manchester City, ambaye anakipiga kwa mkopo wa muda mrefu katika klabu ya Torino, Joe Hart, ili aweze kuwa mrithi wa nyota wao, Thibaut Courtois.

Hatua hiyo ya Chelsea inasemekana kuja baada ya Courtois kuendelea na msimamo wake wa kuwa na ndoto za kutaka kurejea nchini Hispania.

Gazeti la The Sun linaeleza kuwa, endapo ataonesha kiwango kizuri kwa sasa anapocheza kwa mkopo, itamfanya kurejea kwenye michuano ya Ligi Kuu England kutokana na kwamba Chelsea na Everton zinamfuatilia nyota huyo mwenye umri wa miaka 29.
Post a Comment
Powered by Blogger.