GIDABUDAY ACHAGULIWA MWANARIADHA WA MWAKA


Sydney Gidabuday amenyakuwa tuzo ya mwanariadha wa mwaka katika mashindano ya Vyuo Vikuu Marekani. Gidabuday anasoma katika Chuo Kikuu katika jimbo la Colorado, (Adam State University) iliyopo pembezoni mwa milima ya Rookies.
Gidabuday ni kijana wa mwanariadha wa zamani wa Tanzania Wilhelm Gidabuday, Sydney alizaliwa Marekani 1996 wakati wazazi wake ambao ni watanzania walipokuwa wakisoma California.
Tuzo hiyo ni kati ya tuzo yenye heshima kubwa katika NCAA – National Collegiate Athletic Association, sambamba na hilo Gidabuday pia ni bingwa mara tatu wa mashindano hayo ya NCAA D2 na pia anashikilia rekodi kali ya dakika 13 sekunde 36 kwa umbali mita 5000 sawa na kilomita tano.
Gidabuday ana uraia wa Marekani kwa kuzaliwa, iwapo Tanzania ingekuwa na sheria ya uraia mbili angeweza kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya 2020 Tokyo Olympic Games.
This coming December I am coming to my mother land; The Land of Kilimanjaro, Serengeti and Magnificent Zanzibar, alisema Gidabuday.
****************************
HII NDO KAULI YA MZAZI WA GIDABUDAY

Gida “  Nitaridhika zaidi   kuona watoto wengi wa kitanzania  wenye umri sawa  na mtoto wangu  wakifanya  vizuri sio  nje ya  nchi tu hata  nyumbani  Tanzania.

 Hivyo  basi  ilikufanikisha  mafanikio haya  nitagombea  nafasi ya  Katibu Mkuu wa chama cha riadha Tanzania( RT) mwaka  huu.

Post a Comment
Powered by Blogger.