Dola milioni moja zatolewa kupambana na utapiamlo.


Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA limepokea ruzuku ya zaidi ya dola milioni moja kutoka kwa mfuko wa Bill na Melinda Gates ili kusaidia kazi ya shirika hilo katika kupambana na utapiamlo kwa watoto.
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Aldo Malavasi.

Fedha hizo zitafidia gharama ya utafiti za kisayansi juu ya ukuaji wa kiafya wa miili ya watoto wachanga katika nchi za kipato cha kati na chini.

Akiushukuru mfuko huo, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa IAEA Aldo Malavasi amesema kuwa kupambana na utapiamlo ni mfano mkubwa wa matumizi ya mbinu za nyuklia katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu.

Matokeo hayo yatasaidia nchi wanachama kupambana na unene wa kupindukia na utapiamlo ikiwemo kukabili udumavu wa mwili.

Mtaalam wa virutubisho wa IAEA Bi Christine Slater amesema kuwa lishe sahihi katika siku elfu moja za kwanza tangu mama anapotunga mimba hadi mtoto mchanga anapotimiza umri wa miaka miwili ni muhimu kwa ukuaji mzuri na maendeleo ya ubongo.
Post a Comment
Powered by Blogger.