CHADEMA wadai wataibua upya sakata la katiba mpya..
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibua tena hoja iliyoonekana kupoa kwa muda mrefu ya mchakato wa katiba mpya baada ya kuagiza vikao vyao vya ndani vianze kuifanyia kazi kwa kuidai kuanzia ngazi ya msingi hadi taifa.

Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vicent Mashinji, alitoa agizo hilo jana alipokuwa Mkuranga, Pwani wakati wa harambee ya kuchangisha fedha za kumalizia ununuzi wa jengo ambalo litatumika kama ofisi ya wilaya ya chama mkoani humo.
Akizungumza katika harambee hiyo, Dk. Mashinji alisema bado dai la katiba iliyopendekezwa katika taifa ni muhimu kwa maslahi ya taifa.
Post a Comment
Powered by Blogger.