Ajali: Wawili Wafariki Dunia 18 Kunusurika
Watu wawili wamefariki Dunia na 18 kunusurika na wakijeruhiwa vibaya
sehemu mbalimba ya miili yao baada ya kufukiwa na kifusi wakati
wakichimba mawe yanadhaniwa kuwa na dhahabu.
Tukio hilo la kusikisitisha na liloacha simanzi kwa wananchi
limetokea usiku wa kuamkia jumatano majira ya saa tano usiku katika
kitongoji cha Ishimba kijiji na kata na Nyamalimbe wilaya na mkoa wa
Geita.
Wakizungumza baadhi ya wachimbaji wamesema kuwa waliofaliki ni Paul Musa (3o)
mkazi wa Msoma Costantine Samweli( 37) mkazi wa Chato na wote walikuwa
ndani ya shimo hilo.
Pamoja na kutokea tukio la wachimbaji hao kupoteza maisha na wengine
kujiruhiwa baadhi ya wachimbaji wameomba serikali ya awamu ya tano
kuwapatia maeneo ya kuchimba na kuwapa dhana za kisasa.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Jonadhani Muogota amesema kuwa watu
waliokuwa kwenye shimo hilo walikuwa ni wengi lakini wengi wao walitoka
mapema na jitiada za kuwaokoa wawili ziaendelea.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Geita mponjli Mwabulambo alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo kwa njia ya simu alikuwa haya.
Pamoja na eneo hilo kudaiwa kumilikiwa na kampuni ya Mwamba Resources
ltd kwa ajili ya utafiti lakini inadaiwa kuwa kampuni hiyo inachukua
asilimia 60 kutoka kwa wachimbaji wadogo huku kijiji kikichukua asilimia
40.