Aga Khan, ORCI kuchangisha 120 milioni za vita dhidi ya saratani


Taasisi ya Saratani ya Ocean Road kwa kushirikiana na Hospitali ya Aghakan zimeandaa matembezi ya hisani kwa ajili ya kuchangisha fedha kiasi cha Sh120 milioni, ili kusaidia kupambana na saratani ya matiti.
Matembezi hayo yamepangwa kufanyika Oktoba 29 kuanzia saa 12 asubuhi kutoka Hospitali ya Ocean Road mpaka Hoteli ya Kunduchi Beach ili kuhamasisha uchangiaji huo.

 

Akizungumza na vyombo vya habari leo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ORCI Dk Julius Mwaiselage alisema matembezi hayo ni juhudi za kuendeleza mapambano dhidi ya Saratani nchini hivyo ushiriki wa wadau wote unahitajika.
"Tunatarajia Mgeni Rasmi atakuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dk Hamis Kigwangalla, malengo yetu ni kuchangia juhudi za serikali katika kutokomeza saratani ya matiti, lakini pia kununua vifaa na vifaa tiba vya kutolea tiba ya kemikali 'chemotherapy'.
Post a Comment
Powered by Blogger.