Vyama Vya Siasa Matatani - Jaji Francis Mutungi


Msajili wa Vyama vya Siasa, Jaji Francis Mutungi amesema chama cha siasa kitakachokiuka taratibu na sheria kitajifuta chenyewe kwa kukosa sifa.


Jaji Mutungi ametoa kauli hiyo baada ya  kutoa ufafanuzi wa kile kilichodaiwa kuwa ana njama ya kutaka kuifutia usajili Chadema.
Juzi, Baraza la Wazee wa Chadema lilisema kuna njama za kukifuta chama hicho zinazopangwa kupitia ofisi ya msajili huyo.
Baraza hilo pia lilimtupia lawama Jaji Mutungi kuwa anafanya hivyo kwa kutimiza matakwa ya watawala kwa kutumia mwamvuli wa Baraza la Vyama vya Siasa.
Hata hivyo, alipozungumza  jana kuhusu tuhuma hizo, Jaji Mutungi alisema wazee wa baraza hilo wana haki ya kufikiria hivyo lakini hakuna kitu kama hicho. “Vyama vya siasa vitajifuta vyenyewe kwa kukiuka sheria na taratibu zinazofanya viendelee kuwapo,” alisema.

Jaji Mutungi alitoa rai kwa wanasiasa kuepuka kuendesha vyama vyao kwa hisia.
 Alisema uhakiki huo unalenga kupima na kujiridhisha kama vyama vilivyosajiliwa vinafuata taratibu za usajili.“Siwezi kusajili vyama vipya wakati hata hivi nilivyonavyo sijavihakiki,” alisema.
Post a Comment
Powered by Blogger.