V.Money Uso Kwa Uso kwenye Stage Moja Na P-square, Kcee

Vanessa Mdee ataungana na wasanii ‘cream’ kutoka Afrika kwenye tamasha la mara ya pili la One Africa Music litakalofanyika jijini Houston, Texas, Marekani, October 22.

Katika show ya October 22, Vanessa Mdee atapanda jukwaa moja na wasanii wakubwa wa Afrika wakiwemo 2Baba,,Flavour, P –Square, D’Banj, Kcee, Mafikizolo, Fally Ipupa na Cabo Snoop,
“Houston we have a PROBLEM!!!!! See you at the Toyota Centre on the 22nd Oct 2016,” ameandika Vee Money.
“Watu wangu wa Houston na miji mingine ya karibu. Nataka kuwaona kwa wingi.”

Hiyo itakuwa show ya pili baada ya ile ya kwanza iliyofanyika July 22, kwenye ukumbi wa Barclays Centre, New York, Marekani na kukutanisha mastaa kama Diamond, Wizkid, Davido,
 Tiwa Savage, Flavour na wengine wengi.
 
ULIIONA HII YA JUX NA VANESSA MDEE WAKIIMBA WIVU LIVE:
Post a Comment
Powered by Blogger.