Video | Mkubwa Fella Awaaibisha Waliosema Anawanyonya Yamoto Band


Mkurugenzi wa kituo cha Mkubwa na Wanawe na Meneja wa Wasanii Saidi fella maarufu kwa jina la Mkubwa Fella jana amezionyesha nyumba 4 alizowajengea Yamoto Band,

Akizungumza na waandishi wa habari Ijumaa hii akiwa Mbande Kisewe, Chamazi jijini Dar es salaam, Fella amesema ameamua kuonyesha nyumba hizo baada ya kuchoka maswali ya watu kuhusu mafanikio ya wasanii hao.
“Leo nimewaita hapa Mbande Kisewe siyo kuzindua ila kuwaonyesha kwa sababu kuna meseji nyingi nazipata, Mkubwa vipi mbona watoto wananenepa wanavaa vizuri, maendeleo vipi, mbona kuna wasanii wamekuja juzi tu, tunawaona wanafanya vitu vikubwa. Kwa hiyo nimewajengea hizi nyumba lakini bado hazijazinduliwa, nataka uzinduzi wake Mh rais mtaafu Kikwete aje azindue na kuwakabidhi hawa vijana nyumba zao,” alisema Fella.
Aliongeza, ANGALIA VIDEO HAP CHINI “Kwa hiyo nataka wale wanaosema Yamoto wananini waone nini kimefanyika, kwa sababu nilikuwa natengeneza kitu kikubwa, siyo vibanda majumba na mlivyoyaona. Kwa hiyo 80% nyumba zimekamika, kuna vitu ambavyo sijamalizia kwa sababu kila mtu najua atataka kuweka manjonjo yake kwenye nyumba yake, kwa hiyo ndani ya miaka mitatu tulichovuna tumekiwekeza kwenye hizi nyumba, ni kubwa naza kisasa kabisa,”

ANAETAJWA KULIVURUGA PENZI LA MASOGANGE NA RAMMY GALLS AGUNDULIKA

Post a Comment
Powered by Blogger.