Ukame Kuinyemelea Nchi Ya Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dk Agnes Kijazi.

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania(TMA), Dk Agnes Kijazi ametoa tahadhari tano za mwelekeo wa msimu wa mvua katika kipindi cha Oktoba hadi Desemba mwaka huu kutokana na mvua chache zinazotarajiwa kunyesha katika maeneo mengi nchini
 
“Mvua zinatarajiwa kuchelewa kuanza na zikianza zitakuwa chini ya wastani, wakulima wanashauriwa kuandaa mashamba na pembejeo mapema na wazingatie ushauri wa maafisa kilimo kwa kuwa waangalifu katika kuhifadhi akiba ya chakula waliyonayo,” amesema Dk. Kijazi.
 
maeneo yaliotaja ambayo yataadhirika kwa kiwango kikubwa katika utabiri huo wa TMA, umeonyesha kuwa ni mikoa ya Singida, Dodoma, Morogoro, Kigoma, Rukwa, Katavi na Tabora ndiyo inayotarajiwa kukumbwa na uhaba wa mvua zaidi na hivyo wananchi wa mikoa hiyo wametakiwa kuchukua tahadhari.

Hata hivyo, katika mikoa ya pembezoni mwa Ziwa Victoria, ikiwemo Mwanza, Kagera, Shinyanga, Musoma, Simiyu na Geita pamoja na mikoa ya Kusini mwa nchi, Lindi na Mtwara, mvua zinatarajiwa kuwepo kwa kiwango cha kuridhisha.

Mbali ya ukame na migogoro ya wakulima na wafugaji, TMA imetahadharisha kuwa, athari nyingine ya kukosekana kwa mvua hizo itakuwa ni mlipuko wa magonjwa kutokana na uhaba wa maji salama sambamba na matumizi mabaya ya mifumo ya majitaka katika miji.

Post a Comment
Powered by Blogger.