Trey Songz Kutembea Kwenye Mdundo Wa DJ Maphorisa.
Msimu wa nne wa Coke Studio Afrika umeanza kipande cha Nairobi Kenya  wanamuziki wa Afrika wanakutana na kufanya Projects tofauti tofauti.
 Kama utakumbuka msimu uliopita Coke Studio walimualika Ne-yo kama mwanamuziki kutoka nje ya Afrika na kufanikiwa kufanya kolabo na  baadhi ya wanamuziki wa Afrika. zali ambalo limewadondokea washiriki wa msimu huu ni kutembelewa na mkali wa ngoma ya “Nana” Trey Songz.


  Trey Songz anatarajiwa kufanya kazi na wasanii Nyashinski (Kenya). Yemi Alade (Nigeria), Vanessa Mdee (Tanzania), Rema (Uganda), Neyma (Mozambique), Serge Beynaud (French West Africa), Lij Michael (Ethiopia), Stonebwoy (Ghana), na Emtee (South Africa).

 Huku DJ Maphorisa wa Afrika Kusini akitajwa kusimama kwenye mdundo.

“Nilikua natamani sana kufanya kazi na wanamuziki wakubwa duniani na najivunia kutajwa kufanya kazi na Trey Songz, acha Afrika Tufanye kitu kuwaonyesha dunia maajabu tuliyonayo/’ Alisema Dj Maphorisa alipoulizwa atajisikiaje atakapofanya kazi na Triga.

Diamond Platnumz Ft Neyo Will You Marry Me. (Live Perfomance Jembeka Festival CCM Kirumba Mwanza)
Post a Comment
Powered by Blogger.