Soko La Kariakoo Limekuwa Mkoa

 
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imelitangaza eneo la Kariakoo kuwa Mkoa Maalumu wa Kodi, ikiwa ni mkakati mmojawapo wa kuongeza wigo wa vyanzo vya  kukusanya mapato kikamilifu.


TRA imechukua uamuzi huo kwa kigezo cha Kariakoo kuwa ni kitovu cha biashara nchini.

Kutokana na uamuzi huo, mamlaka hiyo imeagiza kila mfanyabiashara wa eneo hilo kumiliki Mashine ya Kielektroniki ya Kodi (EFDs).

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi TRA, Richard Kayombo alisema katika kutekeleza hilo mawakala wote wa EFDs wamefungua ofisi ya pamoja jengo la Al-Falah lililopo Mtaa wa Msimbazi
Post a Comment
Powered by Blogger.